Bujumbura. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe juzi alikutana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza na kumwachia maswali manne atakayoyajibu katika kikao cha dharura cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kilichoitishwa na Rais Jakaya Kikwete ili kuokoa hali ya machafuko yanayohofiwa kutokea Burundi.
Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Mei 13, mwaka huu na kuhudhuriwa na marais wa jumuiya hiyo, kitajadili hali ya kisiasa Burundi.
Hofu ya machafuko imejitokeza baada ya Rais Nkurunziza kutaka kugombea
tena katika uchaguzi ujao, jambo linalopingwa na vyama vya upinzani na
wanaharakati nchini humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni