Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi cheti cha Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyo zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana.
Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora katika Bara la Afrika katika kundi la Majiji ya Kati na kuyabwaga majiji mengine mbalimbali.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (The United Cities and Local Government of Africa- UCLGA) na kupewa jina la Rais wa Angola 'President Jose Eduardo Dos Santos- Africa Mayors Award' ni za mara ya kwanza kufanyika Barani Afrika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni