Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) Bw. Martin Kobler akiwafariji walinzi wa amani kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) wanaohudumu katika Misheni ya MONUSCO ( DRC) kufuatia shambulio lililotokea siku ya Jumanne huko Ben,i Magharibi ya Jimbo la Kivu. Katika shambulio hilo na ambalo limelaaniwa vikali na Katibu Mkuu, Ban Ki Moon, walinzi wawili wamepoteza maisha na wengine 13 wamejeruhiwa.
Na Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amelaani vikali kuuawa kwa walinzi wawili wa amani kutoka Tanzania wanaohudumu katika Misheni ya Kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO).
Walinzi hao wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa na kundi la waasi linalosadikiwa kuwa ni la Allied Democratic Forces ( ADF), shambulio hilo limetokea siku ya jumanne katika eneo la Beni, Magharibi ya Jimbo la Kivu ambapo walinda Amani wengine 13 wamejeruhiwa.
Shambulio hilo limetokea wakati kikosi hicho cha walinzi wa Amani kutoka JWTZ wakielekea kutoa ulinzi kwa wananchi na ndipo waliposhambuliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni