Shirika
linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga
ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii
ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja
wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa
shirika hilo, agizo hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege
nchini Kenya na kuwa anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya
rais Obama itakapokuwa imetua.
Shirika hilo
limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote ya ndege na pia kampuni zote
za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa safari za ndege kadhaa
zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili wakati rais Obama
atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia kwa muda wa dakika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni