Kijana mmoja, Omary
Ramadhani, 28, (pichani) mkazi wa Sinza Madukani, Dar amenusurika kifo
baada ya kupata ajali ya kugongwa na ‘Break Down’ alipokuwa
akiendesha Bajaj katika makutano ya Barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan
Mwinyi, Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa masikitiko, Omary alisema kuwa alipogongwa na gari
hilo hakuweza kujitambua kwani hata wasamaria wema walivyomchukua na
kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walijua alifariki
dunia hivyo wakamuingiza moja kwa moja mochwari, lakini kwa bahati nzuri
alitokea nesi mmoja aliyeshauri asiwekwe kwanza kwenye friji mpaka
apimwe.
Akiendelea kuzungumza kwa tabu kutokana na maumivu ambayo anayo,
Omary alisema baada ya nesi huyo kumpima aligundua alikuwa akipumua kwa
shida.
Alisema hata ndugu zake walijua ameshafariki dunia kutokana na
alivyokuwa, kwani alivunjika mgongo mara sita na mfupa wa mkono ulitoka
nje na kupasuka kichwani jambo lililosababisha kuvuja damu nyingi.
Alifafanua kuwa kutokana na hali yake, alikimbizwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi ambapo baada ya siku tatu alizinduka na walipokuja
ndugu zake aliwauliza alikuwa wapi, walipomuambia Muhimbili alizimia
tena.
Alisema alipata matibabu kwa muda wa miezi sita ndipo aliruhusiwa
kuondoka lakini alitakiwa atoe shilingi 1,000,000 kwa ajili ya tiba
maalum kwenye mashine ambayo siijui jina, lakini nimeshindwa kuzipata na
ndugu zangu ni walalahoi.
Omary alisema hivi sasa bado ana matatizo, haja ndogo haitoki
sawasawa na akienda maliwatoni huchukua zaidi ya saa moja kwani mkojo
hutoka kidogokidogo na kumsababishia maumivu makali ambapo haja kubwa
anapata mara moja kwa wiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni