Spika
wa bunge Mhe Anne Makinda ameongoza mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma katika
kumuaga na kumzika aliyekuwa mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Dodoma marehemu
hajat Mariam Mfaki aliyefariki dunia jumanne hii kwenye hosipitali ya rufaa ya
mkoa wa Dodoma kutokana na kuugua na maradhi ya saratani ya damu kwa muda
mrefu.
Katika
risala yake kwa waombolezaji spika Anne Makinda amemuelezea marehemu hajat
Mariam Mfaki kuwa alikuwa kiongozi muwajibikaji ambaye alitumia muda mwingi
kushughulikia matatizo ya wananchi na kuyafikisha katika sehemu husika bungeni.
Akisoma
risala ya marehemu kwa niaba ya katibu wa bunge mkurugenzi msaidizi huduma kwa
wabunge Suleiman Mvunye amesema kabla ya marehemu kuwa mbunge alifanya kazi
mbalimbali za kuhudumia jamii akianzia na afisa maendeleo wizara ya tawala za
mikoa na serikali za mitaa kuanzia mwaka 1965.
Mbali na
ubunge wa viti maalum marehemu pia aliwahi kushika wadhifa wa katibu wa umoja
wa wanawake Tanzania UWT na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM NEC wilayani humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni