Watu wengi
wamekuwa wepesi sana kukimbilia kwa rafiki zao ili kuomba msaada wa
mawazo ya nini wafanye kwenye mapenzi. Imani iliyojengeka kwa watu wengi
katika jamii yetu ni kuwa ushauri ni kitu muhimu sana kwa kila hatua.
Kwa mtazamo wa
haraka haraka unaweza kuishia kwenye ukomo huo wa fikra na kuamini juu
ya ushauri wa mtu kukufikisha mahali sahihi kwenye mapenzi. Unapokerwa
na mpenzi unakimbilia kushauriwa na wakati mwingine hata unapotaka kuoa
au kuachana na umpendaye, unamuomba rafiki yako ushauri.
Je, umeshawhi
kufikiria hasara za kuomba ushauri wa kimapenzi kwa rafiki yako? Hebu
ungana nami wiki hii ili nikumegee kidogo hasara za ushauri.
UTAKUPOTOSHA
Ni wazi kwamba
kipimo cha uelewa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
Ifahamike kuwa, uhodari wa mambo nao hutofautiana, mtu anaweza kuwa
mahiri katika siasa na akaaminika kwenye jamii, lakini ukimpelekea suala
la mapenzi anakuwa hajui kitu, hivyo ni rahisi kukupotosha.
Uchunguzi
unaonyesha kuwa, wapenzi wengi sana hupotoshwa na rafiki zao wasiokuwa
na uelewa wa kutosha juu ya tatizo au suala husika la kimapenzi. Ni vema
kuwa makini unaposhauriwa.
UTARAHISISHA MAMBO
Mara nyingi
washauri huwa si wao wanaokabiliana na mambo, hivyo ni rahisi kwao
kupima vitu kwa juu juu tu na kushauri kirahisi rahisi. “Vipi kakupiga
namna hii, aaa huyu si mwanaume kwa kweli ni bora ukaachana naye.”
Anasema ni bora kuachana naye kwa sababu haumizwi na kuachana,
unayeachana ni wewe anayekushauri.
“Mkubali tu
bwana unalaza damu, hiyo tabia yake ya uhuni atabadilika, shosti unataka
kuacha bahati ipite?” Kwa mshauri ni rahisi kusema hivyo lakini kumbuka
ukubwa wa tatizo hatimaye utakabiliana nao wewe. Hii ina maana kwamba,
unapofikiria kuhusu ushauri ufikirie pia kuhusu kushauriwa jambo
kirahisi, ukiuvaa mkenge mwenye kuumia utakuwa ni wewe.
UTAKUGEUZA
Ulimwenguni kuna
aina zaidi ya 1000 za mapenzi na kila mmoja anatajwa kupenda kwa staili
zake. Mapenzi ni kama chembe hai nyekundu zilizopo kwenye damu ya
mwanadamu ambazo zinaelezwa na wataalamu kuwa hazifanani hata kidogo.
Uzoefu unaonyesha kuwa, washauri wengi hushauri kwa uzoefu wao, lakini
je ni sahihi uzoefu huo uwe msaada kwa mtu mwingine?
Jibu ni hapana,
kinachotokea mara nyingi kwenye ushauri ni mtu kumfanya mwenzake awe
kama yeye alivyo, yaani apuuze aamue na apende kama staili yake, jambo
ambalo haliwezekani kabisa kwenye mapenzi. Vipi Juma ageuke ghafla awe
kama Hassan kwenye suala la mapenzi? Ushauri ni muhimu lakini upime kama
unalingana na matakwa yako.
UTAKUONDOLEA UJASIRI
“Kwa maelezo
hayo mumeo ni malaya sana, naona itakuwa vigumu kumbadilisha, ni bora
ukaanza maisha yako kwa sababu kuna siku hali itakuwa mbaya.”
Huu ni ushauri
ambao unaweza kumuondolea mtu ujasiri wa kukabiliana na tabia ya mumewe
hadi kufikia hatua ya kumsaidia akaachana na tabia zake mbaya.
Ushauri huondoa
ujasiri wa kukabili tatizo hasa pale anayekushauri atakapolipeleka suala
lako kwenye njia ngumu isiyokuwa na ufumbuzi. Ikumbukwe kuwa anayeamini
kushindwa ni mshauri lakini wewe kama mwanamke unaweza kusimama kutetea
penzi lako na kuliweka sawa mpaka jamii ikasema: “Jamani huyu dada
kamrekebisha kweli mumewe, hakuwa hivi alikuwa mlevi lakini sasa kaacha
pombe.
UTAKUNYIMA FURSA
Kwenye mapenzi
kuna fursa nyingi za mafanikio ambazo unaweza usizipate ukiwa mtu wa
kusikiliza sana ushauri wa watu. Kuna wakati ambao unatakiwa usimame
wewe kuamua kumpenda mtu ambaye jamii inaona kama utapotea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni