.

.

28 Julai 2015

TUNDU LISSU: UKAWA TUNAMSIMAMISHA EDWARD LOWASSA URAIS 2015

Kumekuwa na sintofahamu ya muda mrefu juu ya nani atakayesimamishwa kuwa mgombea urais kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA kutokana na vuta nikuvute inayoendelea ndani ya umoja huo kati ya vyama vinne vinavyounda UKAWA,CHADEMA, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD.
Aliyekuwa mtiania wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa akihusishwa sana na kuisimamia nafasi hiyo ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haswa baada ya kuamua kuhamia CHADEMA baada ya jina lake kukatwa katika mkutano mkuu wa CCM, mjini Dodoma.

KItendawili kilichokuwa katika vichwa vya watanzania wengi ilikuwa ni nani atakaye simama kugombea urais kupitia UKAWA, kitendawili ambacho mbunge wa Singida Mashariki, mhe. Tundu Lissu amekitegua kwa kumtaja Edward Lowassa kuwa ndiye mgombea atakayesimamishwa na UKAWA kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge utakaofanyika oktoba 25, 2015. Mtandao huu umemnukuu Tundu Lissu kama ifuatavyo:
Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
Lowassa: Namshukuru mke wangu Regina, wanangu na wanafamilia katika kipindi hiki kigumu kilichojitokeza.
Lowassa: Nawashukuru wanaCCM waliojitokeza kuniunga mkono wakati nikitafuta wadhamini.
Lowassa: Kilichotokea Dodoma, ni kupora madarakani ya kamati kuu, waswahili wanasema kubaka madaraka.
Lowassa: Chuki na roho mbaya zilitawala licha ya mimi kuwa mgombea mwenye ushawishi na anayekubali zaidi kuliko wote
Lowassa:Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kudanganya nafsi yangu na Watanzania kuwa bado nina imani na CCM
Lowassa: Sijakurupuka kwa uamuzi huu, nawaomba watanzania wajiunge na UKAWA katika Safari ya Matumaini.
Lowassa: Wanaoogopa kisasi wamefanya madhambi gani? Waulizeni..mimi ni Mkristo,sina kisasi..waende wakatubu kwa Mungu wao
Lowassa: CCM Si baba yangu wala Mama yangu. Watanzania kama wameyakosa mabadiliko ndani ya CCM, basi watayapata nje ya CCM.
Lowassa hatimaye amemaliza rasmi kujiunga na CHADEMA na watu sasa wanashangilia wakiimba
- See more at: http://www.fichuotz.com/2015/07/kauli-za-lowassa-mbele-ya-ukawa-na.html#sthash.GbMm3fSV.dpuf

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni