Serikali
imebaini wizi wa takribani shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama
World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi
na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa
kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.
“Kufuatia
upotevu huo Serikali imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi
Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi
utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha usalama mtandaoni ili
kubaini mtandao mzima uliohusika ” alisema Prof.Mbarawa.
Aidha aliongeza
kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya
kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale
anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa
tena.
Prof.Mbarawa
anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo
la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi
na waadilifu.
“Siku mbili
zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini
mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika
hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote
wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.
Vilevile
aliongeza kuwa Serikali imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika
hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama
inavyotakiwa.
Prof.Mbarawa
ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa njia ya mtandao kwa kuwa
sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha
kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa
hatua stahiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni