Katika
kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga
kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) kwa
mujibu wa Kanuni ya 117 (9) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa
na Serikali katika Mkutano wa Pili wa Bunge uliomalizika Februari 2016.
Mikutano hiyo ya
kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Sheria Ndogo inatarajiwa kufanyika
Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2016 na Jumanne tarehe 5 Aprili, 2016 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es
Salaam. Sheria Ndogo ambazo Kamati inakaribisha wadau na umma kwa ujumla
kutoa maoni yao ni pamoja na zifuatazo:-
The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2015
The Public Private Partnership Regulations, 2015
The Copyright and Neighboring Rights (Copyrighted Works – Communication to the Public) Regulations, 2015
The National Examinations Regulations, 2015
The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ General Welfare, Conduct and Disciplinary Matters) Regulations, 2015
The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ Performance Assessment) Regulations, 2015
The Fire and Rescue Force (Fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015
Sheria Ndogo
zilizotajwa hapo juu pamoja na nyingine ambazo zinashughulikiwa na
Kamati, zinapatikana kwa kupakua (downloadable) katika tovuti ya Bunge
la Tanzania ya www.parliament.go.tz pamoja na tovuti ya Serikali ya
www.tanzania.go.tz
Aidha, maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au barua pepe kwa anuani ifuatayo:-
Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,
L. P. 9133, DAR ES SALAAM
Barua pepe: cna@bunge.go.tz
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni