Rais wa Marekani Barack Obama ameanza ziara ya kihistoria nchini Cuba,
akiwa ndiye rais wa kwanza wa Marekani kuzuru taifa hilo katika
kipindi cha miaka 88.
Ziara hii ya siku tatu ndiyo kilele cha mazungumzo ya miaka miwili
yaliyonuia kurekebisha uhusiano kati ya Marekani dola kubwa zaidi
duniani na jirani yake yenye mfumo wa ujamaa.
Rais Obama atakutana na Rais Raul Castro. Punde baada ya kuwasili
Obama alitembea kwenye barabara za mji wa kale wa Havana na pia
kuwahutubia wafanyikazi wa ubalozi mpya wa Marekani.
Kiongozi huyo amesisitiza ziara yake inatoa nafasi kushauriana na raia
wa kisiwa hicho.
Pia ameahidi kuangazia masuala ya haki za binadamu, kuwepo mageuzi ya kisiasa japo maafisa
wa Cuba wamesema hakuna ajenda ya kujadili vile nchi hiyo inaweza
kukubalia vyama vingi vya kisiasa. Cuba inataka zaidi kuondolewa
vikwazo vyote vya kiuchumi na Marekani.
Baada ya kuwasili Cuba, Rais Obama aliandika kwenye Twitter
akiwasalimu raia wa Cuba na kusema anasubiri kukutana nao na kusikia
kutoka kwao.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni