April 19 2016 wawakilishi wa Tanzania
katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa (CAF) klabu ya Azam
FC ilishuka mjini Rades Tunisia kucheza mchezo wake wa marudiano wa
klabu Bingwa barani Afrika dhidi ya klabu ya Esperance ya Tunisia.
Azam FC ambao mchezo wa awali uliochezwa
Chamazi Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa goli 2-1, wamekubali
kipigo cha goli 3-0 katika mchezo huo wa marudiano. Kabla ya mchezo huo
Azam FC walikuwa wakihitajia ushindi au sare yoyote ya magoli ili waweze
kusonga mbele.
Baada ya kuondolewa katika michuano hiyo
klabu ya Azam FC, Tanzania inabakia na muwakilishi mmoja pekee katika
michuano ya kimataifa, ambaye ni klabu ya Dar esa Salaam Young Africans
ambayo April 20 itacheza mchezo wake wa marudiano na wenyeji wake Al
Ahly.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni