Na Msuli Mwaijengo Kyela Mbeya
ZAIDI ya Madereva 300 wa Boda boda Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, wameamua kukusanyika na kuitisha mkutano wa pamoja na Jeshi la polisi kitengo chaUsalama barabarani na Maofisa wa Takukuru wilayani humo, ili kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabiri,ikiwemo Rushwa na Vitisho wanavipata wawapo barabarani.
Wakizungumza jana kwenye mkutano huo madereva hao,wamelishutumu jeshi la Polisikitengo cha usalama barabarani wakidai kuwa wamekuwa wakitozwa faini za mara kwa mara huku listi wanazo andikiwa kama faini zikiwa na utata na kuwa wamedai wakipata vitisho vya kupelekwa mahakamani kama chambo ya kuwapatia rushwa.
Gwani Anyosisye na Ebron Mwaipape madereva wakizungumza kwa nyakati tofauti kupitia mkutano huo,walisema kero kubwa inayowakumba ni kutozwa faini kubwa sawa na gari huku wakipewa lisiti feki na kuwa endapo ukitaka kutoa malalamiko wanatishia kukupeleka mahakamani kitu ambacho ni kinyume na taratibu.
Ambakisye Mwaipyana katibu wa umoja huo,alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wanachama jinsi wanavyo pata usumbufu kutoka kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuwatoza faini za mara kwa mara kwa makosa yakutafutiza huku wakiathiri shughuri za kujitafutia kipato kwa madereva hao.
Widle Mwasika Mwenyekiti wa umoja huo,alitaka kupatiwa ufafanuzi kuhusu changamoto zinazowakabiri hasa za kulazimishwa kujiunga na bima ya afya bila kupatiwa elimu,tozo zisizo na tija,vitisho wavipatavyo kwa askari wa barabarani pamoja na kupatiwa ufafanuzi kuhusu kutozwa faini sawa na magari.
Alisema pikipiki inabeba abiria mmoja,gari linabeba zaidi ya abiria 20 lakini faini inakuwa sawa na kwamba lengo kuu la wao kuitisha mkutano huo kwa kuvishirikisha vyombo husika ni kutaka kupata suruhu ya kisheria kuhusu manyanyaso wanayoyapata na kujua sheria zinasemaje ili waweze kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.
Aliongeza kuwa ikitokea dereva amegonga mtu polisi wa barabarani wamekuwa wa kwanza kuhoji bima wakati wao hawahusiki na bima na kama inatakiwa kulipa faini ukikabidhi leseni kama dhamana ili uende kutafuta pesa ya kulipa wanagoma wamekuwa wakikamata pikipiki na leseni kitu ambacho kinawakosesha uhuru wa kufanya kazi.
Akijibu tuhuma hizo kupitia kikao hicho,mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilayani humo,Leogard Damian alisema faini zote zinatakiwa kutolewa lisiti za karatasi za njano na kama zimekwisha zinatumika nyeupe kama dharula na kuwa madereva wate wanatakiwa kukata bima ili wakimgonga mtu bima ndiyo itumike kumtibu na si vinginevyo.
Akitoa ufafanuzi kuhusu sakata hilo,Afisa uchunguzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani humo,Mponda Mfaudhi alisema kitendo cha askari kupokea rushwa au kuonyesha viashiria hivyo ni kosa kisheria na kuwataka madereva hao kutoa ripoti kwenye ofisi hiyo pindi wanapoombwa rushwa ili sheria ichukue mkondo wake.
Kutokana na hali hiyo,umepatikana muhafaka wa kufanya mkutano kama huo kwa kuwakutanisha walengwa wote ambao ni watu wa bima,jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani,Takukuru na wadau mbalimbali ili kupata tiba ya tatizo hilo ambapo kwa sasa madereva hao wanaendelea na shughuri zao kama kawaida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni