Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silahaaina ya panga ambalo linadaiwa kutumiwa na majambazi hao . |
Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
JESHI la Polisi mkoani Mbeya limewauwa
watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rsasi.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo
Mwambelo amesema tukio hilo limetokea April 27 mwaka huu saa 2 usiku , huko
katika kijiji cha Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .
Amesema watu watano wanaosadikiwa kuwa ni
majambazi wakiwa na bunduki moja ya aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na
risasi 26 kwenye magazine , walifika kijijini hapo kwa lengo la kufanya
uhalifu kwenye duka la jumla la kuuzia vinywaji mali ya Ndugu Hamis Mkazi
wa eneo hilo la Matundasi Chunya..
Kamanda Mwambelo , amesema watu hao ambao miili yao
imehifadhi kwenye chumba cha mochwari katika hospitali ya wilaya ya
Chunya , majina na makazi yao bado hayajajulikana.
Akifafanua, amesema taarifa za siri kutoka kwa raia
wema zilifikia jeshi la polisi na ndipo askari polisi walipofika kwenye eneo la
tukio.
“Baada ya polisi kufika katika eneo la tukio watu
hao walistuka kuwa wanafuatilwa na askari polisi na hivyo kuanza kukimbia
kuelekea kijiji cha Matondo kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili
MC 761. AFS aina ya Sanlag yenye rangi nyeusi”,amesema Mwambelo .
Amesema walipoona Polisi wanawakaribia walianza kurusha
risasi hovyo hewani ambapo jambazi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa
risasi mguuni na tumboni na kufariki dunia ambapo majambazi wanne walifanikiwa
kutoroka .
Amesema kutokana na hali hiyo jeshi hilo la polisi
lilianzisha msako usiku huo na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine
wawili ambao huku wengine wakitoroka ambapo msako mkali unaendelea ili
kuwakamata wahalifu hao.
Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana
bunduki moja aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120
ikiwa na risasi 27 kwenye magazine. Pia pikipiki iliyokuwa
iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea kupatikana pamoja na panga .
Mwambelo alitoa wito kwamba wananchi
waendelee na moyo huo huo wa kuwafichua watu wanaowatilia shaka ili waweze
kudhibitiwa mapema kabla ya kufanya uhalifu sanjali na kufika katika hospital
ya wilaya ya Chunya kwa lengo la kufanya utambuzi wa miili ya majambazi hao
kwani majina yao bado hayajatambulika.
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni