Mbeya city fc yaibuka na ushindi wa magoli manne kwa
sifuri dhidi ya Coastal Union kutoka Tanga katika uwanja wa sokoine mjini
Mbeya,ambapo mpira ulianza kwa kasi huku timu zote mbili zikiwa zinashambuliana.
Goli la kwanza la timu ya Mbeya city fc lilifungwa mnamo
dakika ya 3 ya mchezo kupitia kwa Salvatory Nkulula,ambapo uzembe wa golikipa
wa Coastal union aliweza kuigharimu timu yake baada ya kuutema mpira uliopigwa
kwa adhabu.
Mpira uliendelea kwa kasi yakushambulina kipindi chote
cha kwanza cha mchezo na goli hilo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza mpaka
pale timu ya Mbeya city fc walipopata goli la pili dakika ya 57 ya mchezo
kupitia kwa Salvatory huku akipokea pasi nzuri kutoka kwa Hassani Mwasapili na
kuipatia timu ya Mbeya city fc goli la pili.
Mchezo safi uliooneshwa na timu zote mbili huku ukiwa
unashuhudiwa na mgeni rasmi waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Mh Nape
Moses Nnauye pamoja na mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh Amos Gabriel Makalla.
Goli
la tatu lilipatikana mnamo dakika ya 74 likifungwa
na Hassan Mwasapili ambapo aliweza kuwainua mashabiki wa timu ya Mbeya
city fc
baada ya kupiga kwa ufundi mkubwa na mpira kuingia moja kwa moja katika
nyavu
za timu ya Coastal union,huku goli la nne likiwekwa nyavuni dakika ya 87
kupitia
kwa Ditram Nchimbi na kukamilisha jumla idadi ya magoli manne Mpaka
dakika 90 zinamalizika Mbeya city fc nne Coastal Union sifuri na mpaka sasa Mbeya city fc inafikisha pointi 27ikicheza michezo 25 huku Coastal union akishikilia mkia wa ligi kuu Tanzania bara akiwa na pointi 19 akicheza michezo 25.
Huku waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Mh Nape
Moses Nnauye akisisitiza katika michezo si sehemu ya kuleta mambo ya chama
pamoja na mambo mengine amabayo yanaweza kudidimiza michezo katiaka nchi ya
Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni