Muonekano wa kivuko cha MV. Malagarasi kilichopo katika eneo la Ilagala
mkoani Kigoma. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100, magari
sita na tani 50 kwa wakati mmoja.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa
tatu kushoto), akipata maelezo ya kivuko cha MV. Malagarasi kutoka kwa
Msimamizi wa Kivuko hicho kabla ya kukikagua. Kulia ni Meneja wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani kigoma Eng. Narcis
Choma na Wa pili kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
akishuka katika Kivuko cha MV. Malagarasi mara baada ya kukikagua na
kuona namna ya kivuko hicho kinavyofanya kazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa
pili kulia), akioneshwa vifaa vya uokoaji katika kivuko cha MV. Malagarasi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(kushoto) akijadiliana jambo na mmoja wa abiria wa Kivuko cha MV.
Malagarasi.
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS, mkoani kigoma Eng.
Narcis Choma (wa tatu kushoto) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), barabara ya
Simbo-Kalya yenye urefu wa zaidi ya Km 200 Kusini mwa Ziwa Tanganyika
itakayoanza kujengwa hivi karibuni wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
akitoa maelekezo kwa wananchi wa Ilagala, Sunuka, Karago, Herembe,
Kapalamsenga, Mgambazi, Lukoma hadi Kashagulu ya namna sahihi ya
kutumia kivuko cha MV. Malagarasi, mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa
kwanza kulia), akioneshwa namna ya huduma za uongozaji ndege
zianvyofanyika katika kituo cha Kigoma. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka
ya Usafiri wa Anga mkoani Kigoma Bw. Godlove Longole na katikati ni
Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe akifatilia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(kulia), akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa
Anga mkoani Kigoma Bw. Godlove Longole wakati alipokagua Uwanja wa
Ndege mkoani hapo. Wa pili kulia ni Mbunge wa kigoma Mjini Mhe. Zitto
Kabwe akifatilia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini
(TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia), wakati wa mkutano na
wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa zao katika mwambao wa Ziwa
Tanganyika, mkoani Kigoma.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL) katika picha ya pamoja
na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(katikati waliokaa). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha
Kazaura.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni