Afisa habari wa City, Dismas Ten, ameiambia Mbeyacityfc.com kuwa, nyota waliosafiri mikoani kwa mapumziko ya sikukuu ya Pasaka wanataraji kuungana na wenzao waliosalia jijini Mbeya siku ya kesho tayari wa mazoezi ya pamoja kuiwinda timu hiyo ya Tanga siku ya jumamosi.
Baada ya mchezo wa Songea dhidi ya Majimaji, Mwalimu Kinnah alitoa siku chache za mapumziko, baadhi ya wachezaji walisafiri mikoani kuungana na familia zao, waliobakia jijini hapa walianza mazoezi siku ya jana na leo pia kama unavyowaona, wachache waliokuwa nje ya jiji wataungana na wenzao kesho, hatuna shaka yoyote kuhusu Coastal Union na tuko tayari kwa mchezo wa jumamosi.Kuhusu hali za wachezaji wote Ten alisema kuwa mkuu wa kitengo cha utabibu, Dr Joshua Kaseko, amethibitisha kuwa hakuna shida yoyote kwa nyota waliokuwa wamesalia kambini wako fiti na wameanza vizuri mazoezi chini ya Kocha Kinnah Phiri.
“Nimezugumza na mkuu wa kitengo chetu cha utabibu na amenihakikishia kuwa hakuna majeruhi yeyote na vijana wako tayri kwa mchezo huku wakiwa na ari kubwa ya kuhakikisha City inaibuka na ushindi ili kujiongezea pointi tatu muhimu na kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi” alisema.
Katika hatua nyingine Ten ameweka wazi kuwa licha ya Coastal Union kuchungulia shimo, City haitakuwa na huruma kwenye mchezo huo kwa sababu inahitaji ushindi pekee ili kupata pointi tatu muhimu zitakazoiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi tofauti na sasa ambapo iko kwenye nafasi ya 13, ikiwa na pointi 24.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni