ANGOLAImekumbwa
na Shambulio la kimtandao kutoka katika kundi la wahalifu mtandao
wajulikanao kama “Anonymous” ambapo tovuti 20 za serikali ya Nchi hiyo
zimefanikiwa kuangushwa na kundi hilo la kihalifu mtandao.
Tukio
hilo lilitokea kufuatia shinikizo la kuachiwa huru watu
17walioshikiliwa nan chi hiyo kutokana na kosa la wakipingana na
uongozi wa raisi wa Nchi hiyo Mh. Jose Eduardo dos Santos.
Tukio
hilo la kushambuliwa kwa tovuti za Nchi ya Angola limepokelewa kwa
Maskitiko makubwa sana na wana usalama mtandao wa Nchi za Afrika na
imeonekana changamoto iliyojitokeza iwe ni funzo kua mataifa ya afrika
bado yanahitaji jitihada za dhati kuhimili vishindo vya wahalifu
mtandao.
NEWS
UPDATES: A Portuguese branch of the Anonymous hacking group says it has
shut down about 20 Angolan government websites in retaliation for the
jailing of 17 youth activists for plotting a rebellion against President
Jose Eduardo dos Santos' government.
GHANAilipata
kuathirika na tukio la kuangushwa tovuti zake mwaka jana kitu ambacho
kilipelekea Nchi hiyo kupitia Makamu wake wa Raisi kujipanga zaidi
kuhimili vishindo vya kihalifu mtandao.Taarifa zaidi kuhusiana na tukio
la Ghana inasomeka kwa ku “BOFYA HAPA”
TANZANIAImepata
kuathirika na tatizo la kuingiliwa tovuti kadhaa kipindi cha nyuma na
kusababisha tovuti husika kushindwa kutoa huduma na mara nyingine
kuingiziwa vitu visivyo faa.
KENYAPia
Ilipata kuathirika kwa kiasi kikubwa kwa tovuti zake kitu kilicho
sababisha baadhi ya tovuti kufungwa moja kwa moja – Tulipata kujadili
hili kwa kina nilipo udhuria mkutano wa usalama mitandao wa Nchi za
Afrika mashariki uliofanyika mwaka jana nchini Kenya.
UGANDA,kuimarisha
amani ya nchi hiyo kipindi cha uchaguzi mwaka Huu ililazimika kufunga
mitandao yake ya kijamii pamoja na mifumo mingine ya kimtandao ikiwa ni
hofu ya amani kuyumba. Huu ni mfano ulio hai wenye mazingatio makubwa
ndani yake.
AFRIKA
kwa ujumla wake matukio kadhaa yamepata kutokea nabado yame endelea
kutokea ambapo ni zao la kutotiliwa mkazo swala zima la ulinzi mitandao
kwa Nchi zetu barani Afika kitu ambacho nadhani imefika wakati
pakatiliwa manani mapendekezo ambayo yamekua yakitolewa ili kuweza
kubakisha bara letu salama kimtandao.
DUNIANIkote
kumeendelea kuzaliwa makundi lukuki ya Kiahalifu mtandao amabapo
yameendelea kusababisha maafa makubwa maeneo mbali mbali Duniani – Mfano
Kundi la “Carnabanak” tayari limefanikiwa kuiba ma bilioni ya
kimarekani hadi sasa kwa mujibu wa Ripoti iliyo wasilishwa mapema mwaka
huu.
Uchumi,
Utamaduni, Siasa, Upatikanaji wa Huduma Muhimu ni kwa uchache tu wa
mambo ambayo yameendelea kuathirika kwa kiasi kikubwa kupitia uhalifu
mtandao.
Juhudi
mbali mbali bado zinaonekana ingawa kiujumla wake Nchi za Afrika bado
zimeonekana kutoa uzito mdogo sana kukabiliana na tishio kubwa la
uhalifu mtandao.
Kumekua
na baadhi ya Nchi za Afrika zilizo fanikiwa kuwa na Sheria mitandao
ambapo baadhi bado zimeendelea kua na changamoto. Kuwapo na Sheria pekee
bado imekua ni changamoto kwani vinavyo takiwa kwenda sambamba na
sheria hizo ili kuweza kufikiwa malengo tarajiwa bado havitiliwi uzito.
Hili
limesababisha uhalifu mtandao kuendelea kutikisa na kuathiri jamii zetu
huku baadhi kushindwa kujua athari hizi zinaweza kupelekea mambo mengi
kujitokeza. Kuyumba kwa Uchumi, Kupoomoka kwa maadili, kutikisika kwa
amani na Kutopatikana kwa huduma muhimu zinapo hitajika ni miongoni tu
kwa uchache kwa kinachoweza kuleta shida ndani ya mataifa yetu ikiwa ni
zao la kukithiri uhalifu mtandao.
Bado
imekua ni aghlab kusikia wakuu wa Nchi za Afrika kuzungumzia maswala ya
usalama mitandao isipokua tu pale wanaposhiriki makongamano ya
kiusalama mitandao.
Natoa
wito kwa Nchi zetu za Afrika kuhakiki zinawekeza zaidi kulinda mifumo
yetu ya kitehama ili kuweza kusababisha athari kubwa zinazotokana na
uhalifu mtandao kutoshika kasi kama ilivyo sasa.
chanzo Vijimambo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni