Shirika la ndege
la Kenya, Kenya Airways limetangaza mpango wa kuwaachisha kazi wafanya
kazi 600 kuanzia Mei mwaka huu ili kuzuia shirika hilo kuporomoka. Kwa
mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo Bw Mbuvi Ngunze, shirika
hilo limekuwa likishuhudia hasara na hatua hiyo inalenga kulifanya
lishindane kikamilifu na kuanza kupata faida. Amesema shirika hilo
ambalo limegubikwa na madeni pia litaangalia upya operesheni zake
ikiwemo safari zake na muundo mzima wa kifedha.Wafanya kazi hao ni
kutoka idara mbali mbali za kampuni hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni