.

.

02 Aprili 2016

MWENYEKITI WA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA KYELA AWAPONGEZA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO.




 Na Msuli Mwaijengo Kyela-Mbeya
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa kyela MH KARISONI BONGO amewapongeza madiwa wa halmashauri ya wilaya ya kyela kwa kutaka kikao cha baraza ili kumjadili mkuu wa wilaya ya kyela THEA NTARA kwa makosa kadha anayo fanya hapa wilayani likiwemo la kumsweka lumande diwani wa kata ya lusungo MH VERONIKA KANYANYILA

Amesema vitendo anavyo fanya mkuu wa wilaya vinarudisha nyuma maendeleo ya wilaya hasa kwa kutengeneza migogoro isiyo ya razima kwa matendo anayo fanya kwa viongozi na wananchi wa kyela wakati huu ni kufanya kazi ili kuleta maendeleo yenye tija

Bongo amesema tatizo la serikali ya awamu ya nne ilikuwa ya kubebana hivyo huyu mkuu wa wilaya alibebwa maana serikali kuu na serikali za mitaa zinatakiwa kuwa na mahusiano linapotokea jambo lazima kuwe na ushirikishwaji

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni