Na Maisha Ambangile Kyela Mbeya
Mapema Mwaka huu Kyela FM ilipotembelea vyanzo vya maji katika mlima living stone Kijiji cha Mapinduzi kata ya Mababu, na Kijiji cha Mbuyu Kata ya Makwale na kukuta vyanzo vya maji hayo vimechakaa tangu mradi wa DANIDA na hakuna anaekumbuka kuangalia.
Halimashauri yetu walau ingetenga bajeti ya ukarabati wa vyanzo hivi kuongeza na kuboresha zaidi ilingane na mahaitaji ya watu waliopo saizi. Nakumbuka Waheshimiwa madiwani vijana Thobias Mwamkonda na Katule Kingamkono walipotembelea vyanzo upande wa Ghana na maeneo mengine lakini mpaka sasa kimya sijui nao wamemezwa na madiwani wa business as usual.
Ipo siku huenda Kyela Itapata maji safi na salama kukiwa na viongozi
watakao tanguliza maslai ya kyela kwanza kuliko ilivyo sasa
Kuna mambo Kyela hayahitaji pesa kubwa ili yaende ila yanahitaji viongozi wabunifu na wawajibikaji ili wilaya isonge mbele.
Kuna mambo Kyela hayahitaji pesa kubwa ili yaende ila yanahitaji viongozi wabunifu na wawajibikaji ili wilaya isonge mbele.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni