Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
amemuagiza Kamishna wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernesti Mangu
kumpandisha cheo askari wa Usalama barabarani ambaye alitukanwa na Mke
wa Waziri wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi.
Rais ameyasema hayo wakati akifungua Kikao cha Makamanda wa Polisi wa Mikoa. Aidha Rais Dr. Magufuli amesema ameshamuonya Waziri huyo ambaye mke wake amemtukana askari wa Usalama Barabarani.
Rais ameyasema hayo wakati akifungua Kikao cha Makamanda wa Polisi wa Mikoa. Aidha Rais Dr. Magufuli amesema ameshamuonya Waziri huyo ambaye mke wake amemtukana askari wa Usalama Barabarani.
Wakati akitoa agizo hilo, rais amesema hakuna kiongozi au familia ya kiongozi iliyoko juu ya sheria.
Chanzo: TBC1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni