WATU wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi ambao wametokea Njombe wameuwawa katika majibizano ya risasi na polisi baada ya kuvamia Pub ya Mama Siyovelwa iliyopo eneo la mtaa wa Ikulu mjini Iringa.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10:45 jioni ya jana baada ya watu hao
kuvamia Pub hiyo kwa lengo la kupora kabla ya raia wema kutoa taarifa
polisi.
Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo hilo wamesema kuwa watu hao walihofiwa mapema wakati wa kuingia eneo hilo ambapo inadaiwa walikuwa watatu na mmoja alijichanganya na Raia na kujificha.
Kazi kubwa iliyofanywa na polisi imefanikisha watu hao wawili waliokuwa na silaha kuuwawa bila raia wengine kujeruhiwa.
Miili miwili ya watu hao wanaosadikika ni majambazi ambao baada ya kupekuliwa wamekutwa na tiketi za basi la Hapy National kutoka Njombe imepelekwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku moja watu wawili kufariki dunia kwa kupigwa risasi na majambazi mjini njombe.
Watu waliouawa ni mlinzi wa shule ya sekondary wende na mwingine alikuwa ni fundi gereje mtaa wa Idundilanga.
Katika tukio hilo mwanafunzi mmoja wa kike wa shule ya wende amejeruhiwa vibaya na mwananchi ambaye anaendelea vizuri baada ya kuruhusiwa toka hospotali kibena.
Majina ya majambazi hao bado hayajafahamika na taarifa kutoka Njombe zinaeeleza kuwa huenda kamanda wa polisi akazungumza na waandishi hapo kesho.
CREDIT KINGS FM RADIO

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni