.

.

14 Juni 2016

DUNGA ATIMULIWA TIMU YA TAIFA. HUYU HAPA ANAYEWEZA KUMRITH

dunga-300x200

Brazil imemtimua kocha wake Carlos Dunga siku ya leo Jumanne baada ya Selecao kushindwa kufnya vyema na kutupwa nje katika hatua ya makundi katika Copa America Centenario.
Peru iliwaondoa Brazil kwa kuwafunga 1-0 shukrani pekee kwa goli lilokuwa limejaa utata siku ya Jumapili ambapo ilionekana kugonga mkono wa mshambuliaji Raul Ruidiaz na kuzama kwenye nyavu.
Lakini kwa namna ambayo wamekuwa wakishindwa kupata matokeo ya kuridhisha ikiwa ni pamoja na hii ya kushindwa ilionyesha dhahiri kuwa matokeo ya Brazil yalikuwa hayatoshi kumhakikishia ajira yake Dunga, hivyo Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) likamwondoa kwenye majukumu yake baada ya kurudi kutoka Marekani siku ya Jumanne.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni