TMF YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI NCHINI KUKIMBIZANA NA TEKNOLOJIA.
MKUREGENZI WA MFUKO WA KUSAIDIA VYOMBO VYA HABARI NCHINI (TMF) ERNEST
SUNGURA ALIYESIMAMA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA UKUMBI WA
FLOMI MJINI MOROGORO.
MOROGORO
Waandishi wa
habari nchini wametakiwa kuendelea kujifunza uandishi wa kisasa unaotumia kasi
ya Teknolojia na kuacha kuandika kwa mazoea kwa kutumia mbinu za kizamani.
Wito huo
umetolewa leo mjini Morogoro na mkurugenzi wa mfuko wa kusaidia vyombo vya
habari nchini Ernest Sungura wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya awali kwa
waandishi wa habari waliofanikiwa kupata ruzuku ya kuandika habari za vijijini.
Sungura
amesema kuwa taaluma ya uandishi wa habari kwa sasa inahitaji waandishi
wanaopenda kujifunza mara kwa mara kwani maendeleo ya matumizi ya teknolojia
kila siku yanabadirika.
Sambamba na
hayo Sungura ameongeza kuwa mwandishi ambaye hapendi kujifunza na akaendelea na
uandishi wa habari wa kizamani atakosa soko la ajira katika ulimwengu wa sasa
unaokimbizana na teknolojia ya mitandao.
Katika hatua
nyingine amewataka waandishi wa habari waliopata ruzuku ya kuandika habari za
vijijini kuzitumia pesa hizo za ruzuku katika malengo yaliyokusudiwa ili
kufanikisha kufikia malengo ya kusaidia jamii hususan za vijijini.
Kwa upande
wake Afisa miradi wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini Dastani Kamanzi amewataka waandishi wa habari
kuandika habari zenye ukweli pasipo kupendelea upande wowote.
Mafunzo ya awali
ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Flomi mjini Morogoro yameshirikisha
waandishi wa habari thelathini waliofanikiwa kupata ruzuku ya kuandika habari
za vijijini kati ya waandishi miamoja arobaini na sita waliomba nchi nzima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni