Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina
akimkaribisha Bi. Awa Dabo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa. Mazungumzo baina yao yamefanyika leo Mtaa wa
Luthuli, jijini Dar es Salaam.
Ujumbe
kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, kutoka kushoto ni Bw.
Nehemia Murusuri, Bi. Getrude Lyatuu na Bi. Awa Dabo, walipomtembelea
Naibu Waziri Mh. Luhaga Mpina hii leo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina
akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa kutoka Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada
ya mazungumzo baina yao.
Na Lulu Mussa
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina
hii leo amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Awa Dabo pamoja na ujumbe
aliombatana nao, Ofisini kwake Dar es Salaam.
Katika
mazungumzo yao ujumbe huo umeonyesha nia ya kufanya kazi kwa karibu na
Ofisi ya Makamu wa Rais hususan katika nyanja ya Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira ikiwa ni pamoja na kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na
nishati mbadala.
Awali
Naibu Waziri Mpina aliwafahamisha kuwa Ofisi yake imeandaa Mpango
Mkakati wa Kitaifa wa kupanda miti nchi nzima na kuwataka wadau wa
maendeleo kuwaunga mkono. “Tunaendelea na jitihada za kupanda Miti mingi
iwezekanavyo na katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga fedha kwa
ajili ya kazi hiyo” alisisitiza Naibu Waziri Mpina.
Aidha,
Naibu Waziri Mpina ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza
kuunga mkono kampeni hii kubwa ya upandaji miti nchi nzima na
kusisitiza kuwa uhai wa viumbe vyote unategema Mazingira hivyo ni vema
kuyahifadhi na kuyalinda kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mheshimiwa
Mpina pia amesema Ofisi yake kwa sasa inafanya marekebisho ya Sera ya
Mazingira na kujenga uwezo kwa watendaji wa ngazi zote juu ya kusimamia
Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 pamoja na kuelimisha Umma juu ya
kampeni ya Usafi ya kila mwisho mwa mwezi.
kwa
upande wake Bi. Dabo amesema kuwa shirika lake limeweka vipaumbele vya
kutekeleza ndani ya miaka mitano ambavyo vinaendana na Mpango wa
Maendeleo wa Taifa, sambamba na kusaidia vikundi mbalimbali katika ngazi
za vijiji juu ya kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira.
Bi Dabo
ameahidi kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais katika jitihada za
kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni