Katika
kutengeneza Msingi mzuri kwa wanafunzi wake na kuwajengea uwezo Chuo
Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya inafanya Maonyesho Makubwa ya Ajira na
Ujasiriamali siku ya tarehe 11 June 2015.
Katika
kufanikisha siku hiyo wataalam na wabobeaji wa biashara na fursa za
ajira wamealikwa kutoa mada na kuonyesha uzoefu wao kwenye ujasiriamali
na utendaji kazini. Watoa mada walioalikwa kwenye Tamasha Hilo ni; Imani
Kajula ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Ruge Mutahaba amba
ye ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Wakili Alberto Msando – Wakili
maarufu wakujitegemea na mjasiriamali, Victor Kikoti Compliance Manager –
LAPF na Ephraim Lwila – MenejawaTawi la CRDB Mbeya. Mgeni Rasmi wa
Kongamano hilo ni Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mh.LuhagaMpina.
Upatikanaji
wa ajira za uhakika imekuwa changamoto kubwa sana kwa vijana wengi
wanaomaliza vyuo Nchini Tanzania hivyo ujasiriamali ni njia moja muhimu
ya kutatua changamoto hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni