.

.

26 Mei 2015

KATIBU WA UVCCM MKOA WA IRINGA ELISHA MWAMPASHI AWATAKA VIJANA KUJITUMA KUAFANYA KAZI

katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa, Elisha Mwampashi wa pili kulia akiwa na katibu mkuu wa UVCCM
Taifa Bw Sixtus Mapunda.
Akizungumza na mtandao huu katibu wa uvccm mkoa wa iringa ELISHA MWAMPASHE alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.
"Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani"alisema ELISHA MWAMPASHE
ELISHA MWAMPASHE ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni