.

.

12 Mei 2015

RAIS KIKWETE AMEMTEUA CP DIWANI ATHUMAN KUWA DCI


Mbeyafm Redio's photo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Kamishna wa Polisi ( CP) Diwani
Athumani Msuya , kuwa Mkurugenzi wa
Upelelezi wa makosa ya Jinai ( Director of
Criminal Investigation) .
Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu
Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya
Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa
wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye
amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna
wa Polisi ( DCP) Valentino Mlowola kuongoza
Idara ya Intelijensia ya Jinai , kujaza nafasi
inayoachwa na Kamishna Msuya .
Kabla ya Uteuzi huu , DCP Mlowola alikuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza . Uteuzi
huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015 .
Imetolewa na;
Premi Kibanga ,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi ,
Ikulu – Dar es Salaam .
12 Mei , 2015

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni