.

.

30 Juni 2015

ALI MOHAMED SHEIN AREJESHA FOMU LEO JUNI 30, 2015

mail.google.commm
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein akionesha Fomu yake ya kugombea kwa Wanachama wake katika hafla ya kurejesha Fomu hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Afisi Kuu Kisiwandui. Picha na Makame Mshenga.
mail.google.commz
Naibu Katibu Mkuu CCM,Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa nasaha fupi za kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed mara baada ya kurejesha Fomu ya kugombea Nafasi ya Urais kupitia chama chake katika Viwanja vya Afisi hiyo. Picha na Makame Mshenga
b
Baadhi ya Wanachama waliomdhamini Dkt. Shein wakifuatilia Hotuba aliyokuwa akiitoa Dkt Shein (hayupo pichani) katika hafla ya kurejesha Fomu iliyofanyika katika Viwanja vya Afisi Kuu Kisiwandui.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein leo amerejesha Fomu ya kugombea Nafasi ya Urais kupitia chama chake na kusisitiza kuwa Utulivu na Amani utaendelea kutawala katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Hatua hiyo imefuata baada ya kutimiza Vigezo na Masharti yaliyowekwa katika Fomu hiyo na kusema kazi iliyobaki ni maamuzi ya Chama chake kumpitisha kuwa Mgombea rasmi.
Dkt Shein ameyasema hayo leo Afisi kuu ya CCM, Zanzibar Kisiwandui alipokuwa akiwahutubia Wanachama waliohudhuria katika hafla ya kurudisha Fomu.
Dkt. Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amesema hatomvumilia Mtu atakayevuruga amani ya Nchi na kwamba Uchaguzi Mkuu usichukuliwe kama ni kigezo cha kufanya Vurugu Nchini.
“Narudia tena Zanzibar itabaki kuwa na Utulivu, Amani na Mshikamano na atakayejaribu kuvuruga basi Vyombo vya Dola vitamshughulikia” Alionya Dkt. Shein.
Amewaasa Vijana kuepuka kushawishiwa kuivuruga Amani iliyopo na kwamba kufanya hivyo kutawapelekea kutiwa katika mkondo wa sheria.
Dkt Shein amefahamisha kuwa yeye na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Kikwete wataendelea kusimamia Amani na utulivu kama jukumu lao la Msingi.
Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa Dkt Shein amesema isitumike kama kigezo cha kuchochea Fujo bali kila mtu afanye wajibu wake kulingana na Sheria zilizopo.
Amesema nchi inaongozwa na Sheria na kwamba kila mwenye haki ya kujiandikisha na kupiga kura atapa haki yake hiyo bila usumbufu wa aina yoyote.
“Nchi inaongozwa na Sheria na hakuna aliyejuu ya Sheria, hata mimi Rais sipo juu sembuse wingine, kila mwenye haki ya kupiga kura atapiga bila bughudha yoyote” alisisitiza Dkt. Shein.
Dkt Shein amewataka Wanachama wenzake kuwa watulivu wakisubiri kumalizika kwa Ilani mpya ya CCM ya Uchaguzi unaokuja.
Awali akimkaribisha Dkt Shein, Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alisema Dkt Shein ametimiza vigezo vyote vinavyohitajika na kwamba furaha za Wanachama walioshiriki katika tukio hilo zinaashiria ushindi katika uchaguzi unaokuja.
Dkt Shein ambaye hana Mpizani katika Chama chake alichukua Fomu June18, na kurudisha leo June 30. Aidha amedhaminiwa na jumla ya Wanachama 450 wa Unguja na Pemba kutoka Wanachama 250 ambao ndio Shati la msingi la udhamini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni