.

.

27 Juni 2015

KINANA AVUNA WANACHAMA WAPYA

????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizokuwa za wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo na vyama vingine mara baada ya wanachama hao kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi cha Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza.
Katibu Mkuu huyo amempokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi , Kinana yuko katika ziara ya kikazi9 ya mkoa Mwanza akimalizia mkoa wa mwisho wa Tanzania baada ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani akipita katika majimbo yote, wilaya zote hapa nchini na nusu ya Kata na vijiji kwa muda wa miaka miwili akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.Kinana amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku akihimiza uhai wa CCM ambapo pia katika ziara hiyo amekuwa akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea magwanda ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi, kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu kushoto wakionyesha magwanda yaliokabidhiwa kwao na Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi kutoka CHADEMA
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu wakiwa tayari kupokea kadi za wananchi waliokuwa wanachama wa vyama mbalimbali wakati alipojiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kisesa wilayani Magu leo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi hizo kutoka kwa wananchi hao kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo wakifungua maji kama ishara uazinduzi wa utumiaji wa maji hayo katika mji wa Magu.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakisubiri kuchota maji mara baada ya uzinduzi huo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati alipozindua kikundi cha wajasiriamali cha Magu alipokitembelea leo.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza Ndugu Anthony Diallo akisalimia wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo uliofanyika kwenye ukumbi wa CCM mjini Magu
????????????????????????????????????
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mkutano kabla ya Katibu Mkuu Kinana kusalimia wananchi mjini Magu.
????????????????????????????????????
Kwaya ya Magu One Thietre kikiimba wimbo maalum katika mkutano huo wa kusalimia wananchi mjini Magu.
????????????????????????????????????
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo akizungumza na wananchi kuhusu kuiagiza mamlaka ya Mapato TRA na kikosi cha Usalama Barabarani kuenda katika wilaya kwa ajili ya kutoa huduma za utoaji wa leseni za uendeshaji vyombo vya moto na kukusanya kodi mbalimbali za vyombo vya moto ili kupunguza urasimu wa huduma hiyo ambazo zimekuwa zikipatikana kwenye miji mikuu ya mikoa peke yake.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua wa nyumba hiyo katika kijiji cha Irungu wilayani magu akiwa ameongozana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo kushoto.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni