WATU watatu
wamefariki dunia katika Kijiji cha Kalagu kwenye mwambao mwa Ziwa
Tanganyika Wilaya ya Kigoma Vijijini kutokana na mlipuko
wa kipindupindi huku wengine 10 wakiwa wamelazwa katika
zahanati ya Gungu.
Akizungumza na
chanzo cha habari Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Leonard Subi,
alisema mpaka jana kulikuwa na wagonjwa 10 waliolazwa katika Zahanati ya
Mwakizega ya wilayani Uvinza na watatu wamefariki dunia.
Dk. Subi
alisema ugonjwa huo umelipuka kwa wananchi wanaoishi mwambao wa Ziwa Tanganyika
kutokana na kuwapo raia wa kigeni kutoka nchi ya jirani
ya Burundi ambao wanakuja nao.
Aliwaomba
wananchi kuchukua tahadhari kutokana na ugonjwa huo kwa kuchemsha maji ya
kunywa, kunawa mikono na kula chakula cha moto.
Idara ya
afya ya mkoa wamejipanga kuweka mikakati ya kupambana na ugonjwa huo na
kuhakikisha maji yote yanawekewa dawa kabla hayajafika kwa watumiaji, alisema.
"Ninawaomba
wananchi waendelee kuchukua tahadhali kutokana na mlipuko huu wa
kipindupindu ambao ni hatari… naomba wananchi wahakikishe wanaweka
mazingira katika hali ya usafi na waache tabia ya kula kula hivyo,”
alisema Dk. Subi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni