Utawala wa Rais Barack Obama wa Marekani unafanya mipango ya kuanzisha kambi mpya ya kijeshi katika jimbo la Anbar nchini Iraq na kuwatuma wanajeshi wa kutoa mafunzo na ushauri kuliimarisha jeshi la Iraq ambalo limekuwa likipambana na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS. Duru zinaarifu kuwa Rais Obama huenda akauidhinisha mpango huo wa kuongeza shughuli za kijeshi nchini Iraq hii leo. Wanamgambo wa IS waliuteka mji mkuu wa jimbo la Anbar wa Ramadi mwezi uliopita na Marekani inapanga kuweka mikakati madhubuti kuukomboa mji huo. Marekani ina wanajeshi 3,100 nchini Iraq wanaotoa mafunzo na ushauri hivi sasa. Rais Obama anatarajiwa kuidhinisha mpango huo wa kutuma majeshi zaidi nchini Iraq mapema iwezekanavyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni