Waasi nchini Syria wameiteka kambi muhimu ya kijeshi kusini mwa nchi hiyo katika jimbo la Daraa baada ya mapambano kati yao na majeshi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad yaliyodumu kwa saa 24 hapo jana. Wapiganaji 2,000 wa makundi mbali mbali ya waasi yaliyoungana wameshiriki katika kuiteka kambi hiyo ambayo iko mpakani na Jordan na karibu na jimbo la Sweida ambalo linadhibitiwa na majeshi ya serikali. Shirika la kutetea haki za binadamu la Syria limethibitisha kuwa kambi hiyo imeangukia mikononi mwa waasi na kuongeza kuwa waasi 15 na wanajeshi 20 wameuawa katika mapambano hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni