.

.

13 Julai 2015

ASKARI WAGONGANA NA BODABODA MBELE YA KITUO CHA POLISI MOROGORO


ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (F.F.U) mkoani Morogoro aliyefahamika kwa jina moja la Mage amevunjika mguu na kupoteza fahamu kwa muda baada ya pikipiki aliyopanda kugongana uso kwa uso na bodaboda eneo la Mji Mpya mbele ya kituo cha polisi.
Afande Mage ambaye amevunjika mguu na mfupa kutoka nje, amepelekwa katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro akiendele na matibabu.
Dereva wa pikipiki aliyokuwa amepanda Afande Mage ambaye pia ni askari polisi aliyefahamika kwa jina moja la Shaibu, hakuumia sehemu yeyote ya mwili wake wakati huo dereva wa bodaboda waliyegongana naye ambaye jina lake halikufahamika ameumia vibaya sehemu ya kichwa za kupoteza fahamu.
Akizungumza na mwandishi wetu, shuhuda wa tukio hilo Siasa Said alisema;
“Hawa maaskari walikuwa wakitokea mjini wakiwa mwendo wa kawaida, huyu kijana wa bodaboda alikuwa akitoka Mwembesongo na alipofika hapa Kituo cha Polisi Mji Mpya wakiwa mwendo kasi alijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso na pikipiki ya maafande hawa.
Afande Mage alivunjika mguu huku Afande Shaibu akinusurika baada ya kuwahi kuruka alipoiona ajali hiyo”
alisema shuhuda huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni