.

.

12 Julai 2015

DENI LA UGIRIKI KUJADILIWA TENA BRUSSELS

Mawaziri wa fedha kutoka nchi zinazotumia sarafu ya euro wanarejelea mkutano wao pamoja na waziri wa fedha wa ugiriki kuhusu makubaliano ya kutoa mkopo kwa nchi ya Ugiriki.
Wakati wa saa tisa za mazungumzo mjini Brussels siku ya Jumamosi Euclid Tsakalotos alishindwa kuzishawishi nchi zingine za ulaya kuwa Ugiriki ina mipango mizuri ya kumaliza tatizo lake la deni.
Serikali ya Ugiriki inaomba mkopo mpya wa karibu euro bilioni 70.
Ujerumani imekuwa ikidai kuwa Ugiriki itaondoka kwa muda kwenye nchi zinazotumia safaru ya euro hatua ambayo inapingwa na Ufaransa na baadhi ya nchi za ulaya zinazo ihurumia Ugiriki.
Mawaziri hao wanatarajia kuwa na mpango kabla ya mkutano wa viongozi wa nchi za ulaya ambao utafanyika baadye hii leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni