.

.

12 Julai 2015

MGOMBEA URAIS CCM KUWEKWA HADHARANI LEO

 Magufuli unakabiliwa kikwazo kikubwa kutoka kwa makada hao wawili wanawake na wanadiplomasia.
Watatu hao walifanikiwa kuingia hatua hiyo ya mwisho ya kupigiwa kura na mkutano mkuu baada ya kuwabwaga makada wengine wawili, Bernard Membe, ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuenguliwa na Kamati Kuu juzi, na January Makamba katika kura zilizopigwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu.. Sasa ni wazi; mmoja kati ya Dk John Magufuli, Dk Asha Rose Migiro au Balozi Amina Salum Ali atapeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu ujao baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu kukamilisha kazi yao ya kupiga kura usiku mwingi wa kumkia leo.
Licha ya mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa matokeo ya kura hizo yatatangazwa leo saa 4:00 asubuhi kuna kila dalili kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk Magufuli ndiye atakayepeperusha bendera ya chama hicho.Lakini ushindi wa Dk Magufuli unakabiliwa kikwazo kikubwa kutoka kwa makada hao wawili wanawake na wanadiplomasia.Watatu hao walifanikiwa kuingia hatua hiyo ya mwisho ya kupigiwa kura na mkutano mkuu baada ya kuwabwaga makada wengine wawili, Bernard Membe, ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuenguliwa na Kamati Kuu juzi, na January Makamba katika kura zilizopigwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu.Awali kabla ya kupigiwa kura na Mkutano Mkuu jana, Kikwete aliwataka wajumbe kumuunga mkono mgombea atakayepitishwa kupeperusha bendera ya chama hicho na kuachana na makundi.Wagombea wapo watatu na wote wana sifa za kuwa Rais. Halmashauri Kuu imewapitisha kwa kujiridhisha na tabia na mienendo yao na atakayepitishwa ataiongoza nchi yetu vizuri. Anatakiwa apatikane Rais zaidi yangu ili tusonge mbele. Tunataka rais atakayefanya mambo zaidi yangu,” alisema JK.Tumevuka hatua ya makundi na sasa tunatafuta mgombea wa chama na si mgombea wa kundi au mgombea binafsi. Wagombea urais waliojitokeza walikuwa 38 na makundi lazima yalikuwa mengi. Tukipata mgombea mmoja makundi yanatakiwa kuyeyuka.”
Hisia za wajumbe kwa Dk Magufuli zilionekana wazi wakati makada hao walipopewa dakika 15 za kujieleza mbele ya Mkutano Mkuu, huku mwenyekiti akiweka sharti la kuzuia kushangilia hata kama wakiguswa. Lakini sharti hilo lilionekana kuwasumbua wajumbe hao na mara kwa mara wakajikuta wakilipuka na kushangilia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni