Aliyekuwa anawania kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho, Profesa Mark Mwandosya amesema atamuunga mkono mgombea yeyote atakayeteuliwa.
Vilevile, Profesa Mwandosya amesisitiza kauli yake ya awali kuwa hatawania ubunge katika Jimbo la Rungwe Mashariki na tayari ameshawaaga wananchi wa jimbo lake.
Hata hivyo, Waziri huyo katika Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) alibainisha kuwa hawezi kustaafu siasa kwa sababu ni maisha ya kila siku kwa binadamu.
Akizungumza katika ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana, Profesa Mwandosya alisema: “Katika nyakati mbalimbali mataifa na binadamu hupita kwenye nyakati za majaribu, njia ambayo Mwenyezi Mungu huimarisha mtu na Taifa iwapo tutaweza kuyamudu. Hiki ndicho kipindi tunachopita sasa kama Taifa.
“Kwa maneno haya sasa napenda na kwa unyenyekevu mkubwa kuwashukuru kwa dhati kabisa wale wote mliotuunga mkono kabla na baada ya kutangaza nia, wakati na baada ya kuchukua fomu za kuomba nafasi hiyo kwa imani kwamba ninakidhi na pengine ninazidi vigezo vilivyowekwa.”

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni