Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inakanusha taarifa zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa Ofisi hii imehusika kuandaa kikao kwa ajili ya kuchangisha fedha za kumuwezesha mmoja wa waliokuwa wagombea wa kiti cha urais kupitia moja ya vyama vya siasa ili fedha hizo zitumike kutoa rushwa wakati wa taratibu za kumpata mgombea wa chama kwa nafasi ya urais.
Ofisi inaviarifu vyombo vyote vya habari nchini pamoja na wananchi wote kuwa hakuna kikao chochote kilichofanyika tarehe 03/07/2015 katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ajili ya kuchangisha fedha za taratibu za uchaguzi.
Aidha, Kanuni za Maadili katika utumishi wa umma haziruhusu jambo hili. 2 Pia, cheo kilichoripotiwa (KAMISHNA) hakipo katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, na anayetajwa kuratibu kikao hicho Bw. Mkwizu ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu na sio KAMISHNA hakuwepo Ofisini toka tarehe 25/06/2015 hadi tarehe 05/07/2015 kwa kuwa alikuwa nchini Estonia katika ziara ya mafunzo kuhusu utekelezaji wa Serikali Mtandao. Hivyo, Ofisi hii inawataka wananchi kupuuzia suala hilo ambalo halina ukweli wowote na kuitaka mitandao ya kijamii kutoandika habari zinazopotosha umma kwa lengo la kuifarakanisha Serikali na wananchi wake hasa katika kipindi hiki cha vuguvugu la kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Suala la kuzingatia weledi ni muhimu ili kutoleta migogoro kupitia habari za uongo, au kuzusha masuala ambayo hayapo. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inasisitiza kuwa inasimamia na itaendelea kusimamia Kanuni, Sheria na Tararibu za Utumishi wa Umma.

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma 14 Julai 2015.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni