CHAMBUZI NEWS
.
14 Julai 2015
BAADHI YA WATU WASHUTUMIWA KUUZA MAENEO VIWANJA VYA JANGWANI BILA UTARATIBU
Watu waliovamia eneo la viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam na kuanza kujiuzia maeneo hayo kwa shilingi laki moja hadi shilingi laki tano kwa kipande, wametakiwa kuondoka haraka katika maeneo hayo mpaka pale uongozi wa manispaa hiyo itakapogawa maeneo hayo kwa watu sahii kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa manispaa ya Ilala Bwana
Isaya Moses Mngurumi, amesema ameshangwazwa na kitendo cha watu kuvamia eneo la Jangwani kabla ya kugawiwa na uongozi kama ilivyopangwa.
Kuhusu upande mwingine, mkurugenzi amesema ameshangazwa na kitendo cha watu kuanza kujenga vibanda huku wengine wakiuziana kwa gharama kubwa wakati lengo ilikuwa ni wafanyabiashara hao kutandika bidhaa zao chini mara tu baada ya kugawiwa maeneo hayo na uongozi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni