.

.

23 Julai 2015

WAATHIRIKA WA MAFURIKO WALALA NJE BAADA YA MAHEMA KUHARIBIKA HUKO MOROGORO

Zaidi ya kaya 260 waathirika wa mafuriko wanaoishi kwenye mahema katika eneo la Mateteni wilayani Kilosa mkoani Morogoro wanaishi maisha magumu kwa kutegema viazi vitamu na wengine wanalazimika kulala nje na familia zao kutokana na uchakavu wa mahema.
Wakizungumza kwa uchungu waathirika hao wamelalamikia kuendelea kuishi maisha magumu kutokana na uchakavu wa mahema ambapo baadhi yao wanalala nje na watoto na kuishi kwa kutegemea viazi vitamu kusukuma maisha ambapo wameomba serikali kuona huruma kwa watu hao kutokana na maisha magumu wanayoishi.
 
Nae mtafiti kutoka taasisi ya naliendele Bernadeta Kimata akizungumza na wananchi hao amesema waliliona hilo na ndio maana wakagawa mbegu za viazi bure kwa wananchi ili kuwezesha waathirika hao kupata chakula kwa muda mfupi kuwawezesha kukabiliana tatizo la njaa ambapo wamewataka walime viazi kwa wingi viwasaidie kupunguza ugumu wa maisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni