.

.

14 Septemba 2015

RAIS KIKWETE AZIAGIZA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU.



Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wananchi inayotekelezwa na shirika la nyumba la taifa (NHC) ili kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini na kati kumiliki nyumba zao wenyewe.
Rais Jakaya Kikwete anatoa agizo hilo wakati akizindua miradi ya nyumba za makazi na jengo la kitega uchumi la Lumumba Complex manispaa ya Kigoma ujiji ambapo amesema baadhi ya halmashauri zimekuwa zikichelewa kugawa maeneo kwa shirika hilo huku zikitoa visingizio lukuki ambavyo mara nyingi vina maslahi binafsi na baadhi ya maofisa.
Kwa upande wake waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mhe william lukuvi amesema kwa kipindi cha miaka 10 ya utawala wa serikali ya awamu ya nne shirika la nyumba la taifa limepiga hatua kubwa huku likiwawezesha wananchi kumiliki nyumba zao wenyewe na kutoa ajira nyingi kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya vijana.
Nae mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba nchini Nehemia Mchechu amesema shirika hilo bado litaendelea kuboresha maisha ya watanzania kwa upande wa makazi bora na ya bei nafuu katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwawezesha watanzania kumiliki nyumba bora na za kisasa ili kujiletea maendeleo wao wenyewe na taifa kwa ujumla

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni