Mkemia mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele.
Na. Jovina Bujulu
Wanafunzi
wanaosoma masomo ya Sayansi kote nchini wameshauriwa kuongeza bidii
katika kujifunza masomo hayo ili kuendana na juhudi zinazofanywa na
Serikali za kuwawezesha wanafunzi hao kujifunza masomo ya Sayansi kwa
vitendo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof.
Samweli Manyele kwenye sherehe ya kuwapongeza wanafunzi 24 wa kidato cha
nne na sita waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa
mwaka 2013 na 2014.
“Kama
wachunguzi wa Serikali ambao hutumia taaluma zitokanazo na masomo ya
Kemia na Biolojia tumeona ni Vizuri kutoa hamasa kwa vijana na Taifa
hili kupenda masomo ya Sanyansi” Amesema Prof. Manyele.
Amesema
Zoezi la kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye
masomo ya Kemia na Biolojia limeanzishwa kutoakana na Wakala ya Mkemia
Mkuu wa Serikali kupewa jukumu la kusimamia Sheria ya Usimamizi na
Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani.
Aidha,
amesema Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kitagharamia masomo ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano kwa walimu na wanafunzi wanne ili waweze
kuimarisha vipaji vyao vya masomo na matumizi ya kompyuta .
Amefafanua
kuwa Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi 24 na walimu 4 kutoka shule
mbalimbali za Sekondari hapa nchini wamezawadiwa vitu mbalimbali
zikiwemo Fedha, Vyeti na Santuri kwa ajili ya kujifunza zaidi masomo ya
Sayansi kwa upande wa wanafunzi na walimu kujifunza mbinu zaidi za
kufundisha masomo hayo.
Kwa
upande wa Wanafunzi waliozawadiwa amesema wanatoka shule za Sekondari za
Feza, Marian, Iliboru, St. Francis na Shule ya Sekondari ya Kata ya
Nyamanoro iliyoko jijini Mwanza.
Sherehe
za kuwazawadia na kuwapa tuzo mbalimbali wanafunzi wa masomo ya Sayansi
zilianzishwa mwaka 2007 chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali, huambatana na
utoaji wa zawadi na tuzo mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri
katika masomo ya Kemia na Bioloji.Chanzo mjengwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni