.
14 Septemba 2015
WATU 12 WAUAWA KIMAKOSA MISRI
Watu 12 wanaripotiwa kuuawa na jeshi la nchini Misri jana ikiwa ni pamoja na watalii kutoka Mexico na raia wa Misri, baada ya kushambuliwa kimakosa kwa kulengwa magari yao wakati wanajeshi walipokuwa wanapambana na wanajihadi magharibi mwa Misri.
Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema Vikosi vya pamoja vya jeshi hilo ambavyo vilikua vikipambana na magaidi katika eneo la Wahat katika Jangwa la Magharibi, walirusha risasi kwa makosa dhidi ya magari mawili madogo yaliokuwa yakisafirisha watalii kutoka Mexico.
Jangwa la magharibi ambalo ni maarufu kwa watalii ni moja kati ya maficho muhimu ya makundi ya kijihadi,pamoja na kundi la dola ya Kiislamu – Islamic State
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni