wadau mbalimbali wakiwa katika sherehe fupi yakumuwaga Rebeka Njulumi.
Rebeka(katikati) akikabidhiwa cheti cha ufanyaji kazi kwa bidii
Picha zote na Robert Eliah
YWCA Mbeya wamuwaga
Rebeka Njulumi ambaye alikuwa afisa mradi wa wajibika Mkoani mbeya,sherehe hiyo
fupi yakumuwaga Rebeka ilifanyika katika ofisi za YWCA zilizozopo eneo la
Mabatini,nakudhuriwa na watu mbalimbali pamoja na wadau wa YWCA Mbeya.
Kwaa upande wake afisa
msaidizi wa mradi huo bwana Elly Bonkey aliweza kumshukuru Rebeka kwa kipindi
chote walichokuwa nae katika kuhakikisha wananchi wanatunza mazingira na
kupanda miti,lakini pia aliweza kumshukuru kwa kutoa elimu ya vikoba kwa kina
mama wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.
Nae mwanafunzi wa
Nzonda haki Mussa Mbugi ambaye ni mwenyekiti wa mradi wa wajibika shuleni hapo
aliweza kumshukuru Rebeka kwa kuwafanya wae mfano bora wa utunzaji mazingira
shuleni hapo hususani kupanda miti na kuweka mazingira katika hali ya usafi.
Katiaka upande wa
kinanamama ambao waliweza kupata elimu ya vikoba waliweza kumshukuru Rebeka na
kumtaka huko aendako akaendeleze mapambano ya kuwatoa watu katika umasiki na
kuwapa elimu ya vikoba ili mradi tu watu wakima cha chini wanufaike na elimu
anayoitoa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni