Vyama kadhaa vya
upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vimeitisha maandamano katika
mji mkuu wa taifa hilo Kinsasha dhidi ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais
uliotarajiwa mwezi Novemba mwaka 2016.Wiki iliopita ,mahakama ya kikatiba
nchini humo ilitaka siku ya uchaguzi huo kuangaziwa upya ,hatua ambayo
wapinzani wanasema ni ya kutaka rais Joseph Kabil kusalia mamlakani zaidi hata
baada ya kukamilika kwa muda wake uliowekwa kikatiba.Mabango yaliobebwa na
vyama hivyo yalisoma ''mabadiliko ya uongozi ni sharti yafanyike''Maandamano ya
kupinga kucheleweshwa kwa uchaguzi huo yalizua ghasia mnamo mwezi Januari na
kusababisha vifo vya takriban watu 36.Bwana Kabila amekuwa madarakani tangu
babaake aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo auwawe mwaka 2001.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni