.

.

11 Februari 2016

CHUI WAFUNGA SHULE 130 INDIA


Zaidi ya shule 130 jijini Bengaluru, nchini India zimefungwa baada ya chui watatu kupatikana wakirandaranda ndanii ya mojawapo ya shule hizo katika kipindi cha siku tatu zilizopita.
Siku ya Jumapili chui mmoja alipatikana akirandaranda ndani ya shule ya Vibgyor na siku mbili baadaye wengine wawili wakapatikana karibu na shule hiyo hiyo. Mmoja wa chui hao alishikwa na maafisa wa wanyamapori lakini wengine wawili bado hawajulikani waliko.
"Kufuatia tishio la chui tumefunga shule 134 katika jiji la Bengaluru. Tutatoa uamuzi iwapo tutazingua Ijumaa," afisa wa serikali ambaye hakutaka kutambuliwa alisema. Visa vya chui kupatikana ndani ya maeneo panapoishi watu vimeongezeka nchini India ambapo kuna zaidi ya chui 14,000.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni