Chama
cha Wananchi CUF cha nchini Tanzania kimekubali kurudi kwenye
mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi wa amani mkwamo wa kisiasa visiwani
Zanzibar, kwa sharti kwamba, mchakato wa uchaguzi wa marudio
usimamishwe.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalimu Seif Shariff Hamad
mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Maalim Seif
ametoa msimamo huo wa CUF baada ya baada ya kukutana na waziri mkuu
mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa ambaye pia alikuwa mgombea wa urais
wa Tanzania wa chama cha CHADEMA chini ya mwavuli wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi UKAWA kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana. Aidha
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza ya Rais wa Zanzibar amekitoa
hofu cha tawala cha CCM na kusema kuwa, haoni sababu ya chama hicho
kuhofia CUF kuchukua madaraka ya serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani
Zanzibar. Alisema chama chake hakina ajenda ya kulipiza kisasi.
Itakumbukwa kuwa, matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi
na madiwani yalifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),
Jecha Salum Jecha siku ambayo tume hiyo ilitakiwa kumtangaza mshindi, na
mwezi uliopita wa Januari, mwenyekiti huyo wa ZEC alitangaza Machi 20
kuwa siku ya uchaguzi wa marudio visiwani humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni