.

.

15 Februari 2016

KINNAH PHIRI AJIGAMBA KUENDELEZA DOZI ASEMA SASA NI ZAMU YA AZAM KUCHEZEA KICHAPO SOKOINE JUMAMOSI

                                      Kocha mkuu wa Mbeya City fc KINNAH PHIRI


                             Mashabiki wa Mbeya city fc

Kocha mkuu wa klabu ya Mbeya City Kinna Phiri ameweka hadharani kuwa vijana wake wamejipanga vyema kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Azam mchezo unaotaraji kupigwa siku ya jumamosi
Akiongea na Chambuzi news katika hotel ya Living stene Mbeya Phiri amefahamisha kuwa hakuna kinachoshindika kuifunga Azam ana kujikusanyia point tatu kufuatia marekebisho aliyoyafanya katika mitindo ya uchezaji ambapo watakuwa wakitumia mbinu zaidi walizozionesha kwenye mchezo dhidi ya Toto African na kuibuka na ushindi ambao timu hiyo tangu ipande ligi kuu haijawai kuupata.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni