Mamlaka ya
chakula na dawa TFDA kanda kati wameteketeza tani za vipodozi, vifaa
tiba na vyakula vyenye uzito wa tani tatu na nusu zikiwa na thamani ya
shilingi milioni kumi na tatu na laki tano ambazo hazitakiwi kutumika
nchini na vilivyo kwisha muda wake wa matumizi.
Akiteketeza
vifaa hiyo afisa mkaguzi wa chakula kutoka mamlaka ya chakula na dawa
TFDA kanda ya kati Bwana Aberl Deule amesema baadhi ya wafanyabiashara
sasa wameanza kubadilisha muda wa matumizi kwenye bidhaa za makopo na
kusababisha wananchi kupata madhara ya kuugua matumbo.
Kwa upande wake
mganga mkuu wa manispaa ya Singida Daktari John Mwombeki amesema pamoja
na wafanyabiashara wengi hufahamu madhara ya kuuza bidhaa za vipodozi
ambvyo vimekatazwa hapa nchini na kupunguza kasi ya kuvileta tofauti na
awali, sasa wamekuwa wakitumia njia ya kuzificha bidhaa hizo tofauti na
awali walikuwa wakiviweka katika mbao za kuuzia.
Mamlaka ya
chakula na dawa kanda ya kati TFDA imefanya operesheni hiyo kwa muda wa
siki kumi katika kata nane na kukagua majengo miamoja themanini na tatu
yakiwemo majengo ya dawa viwanda vya chakula na machinjio ya manispaa ya
Singida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni